Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Siku ya hukumu yaja, na sisi zote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu, na hapo patakuwa na vitabu viwili, mmoja itakuwa ni ya waliyo tenda dhambi, na kitabu cha pili itakuwa ni ya watakatifu.
Kwenye kitabu cha UFUNUO WA YOHANA 20:12,15 inanena kuhusu vitabu hivi, kwenye msitari wa 12 Yohana amenakili akisema; "Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi, na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao" Hii ina maana kwamba kila mtu ,uwe ni mwokovu ama hata kama ujaokoka, zote tuta kusanyika mbele ya kiti cha enzi kuuhukumiwa.
Katika msitari wa 15 inasema; "Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto". Je, jina lako limeandikwa katika kitabu kipi?
Katika kitabu cha LUKA 10:17-18,20, Biblia inasema; Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha,wakisema, bwana hata pepo wanatutii kwa jina lako,akawaambia,nilimwona shetani, akiangukakutoka mbingunikama umeme. Msitari wa 20 inasema; "Lakini msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii, bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni". Ili jina lako liandikwe katika kitabu cha uzima, ni sharti uokoke, ujazwe Roho Mtakatifu, utembee na Kristo kwa haki, na kila mara,fanya mapenzi ya Mungu.
Katika kitabu cha MATHAYO 7:21 Inasema; Si kila mtu aniambiaye , Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa Mbinguni ; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
Wapendwa, tunastahili kufahamu kwamba, chochote kila mtu afanyacho kina rekodi kule mbinguni; kile utendacho, kinacho toka kinywani mwako, na mwenendo wako, yamenakiliwa katika kitabu aidha cha uzima, au kitabu cha mauti. Je jina lako limenakiliwa katika kitabu kipi, je baada ya kuondoka duniani, utakuwa wapi?
Okoka, ukombolewe, ujashwe Roho Mtakatifu na utende haki(fanya mapenzi ya Bwana) ili jina lako liandikwe katika kitabu cha uzima.