Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Je unaelewa mapenzi ya Mungu kwetu? Wengi wanajiuliza maswali mengi kuhuzu mapenzi ya Mungu.
Warumi 12:2; Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Ili uelewe mapenzi ya Mungu, ni lazima nia yako ufanywe upya; kwa maneno mengini lazima ufanyike kiumbe kipya kwa kuokolewa na kujazwa Roho mtakatifu. Maana hauwezi kuelewa mambo ya Roho kama hauna Roho mtakatifu, na hauwezi kumpokea Roho mtakatifu kama hauja mpokea Kristo Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako.
1 Wakorintho 2:10-11; Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho uchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila Roho ya binadamu iliyo ndani yake? Hivyo ndivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho ya Mungu.
Kwa hivyo, ili ufahamu mapenzi ya Mungu, ni lazima ujazwe Roho mtakatifu, maana ni Roho ya Mungu pekee aliye na uwezo wa kufunua mambo ya sirini pake Mwenyezi Mungu.
1 Wathessalonike 4:3-4; Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; Kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima.
Mapenzi ya Mungu kwetu ni; 1. Kuishi maisha matakatifu (Wakolosai3:5), 2. Tuwe watendaji wa neno la Mungu (Yakobo1:22), 3. Kumpokea Kristo Yesu kuwa Bwana na mwokozi wako(kuokoka; Yohana 3:3), 4. Kujazwa Roho Mtakatifu (Waefeso 5:18), 5.Uweze kufanikiwa (Kumbukumbu la Torati 29:9), 6.Uwe na afya njema(3 Yohana1:2)
Naomba mapenzi ya Bwana wetu Yesu Kristo ifanyike maishani mwako.