Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
YOSHUA 6:1-4
Haya ya 1.Tunapo soma bibilia katika kitabu cha Yoshua, tuna jifunza ya kwamba, Yeriko ulikuwa umefungwa kabisa kwa sababu ya wana wa Israeli; hapana mtu aliyetoka wala hapana mtu aliyeingia. Inamaanisa kwamba kuliwekwa KIZUIZI ili kuzuia wenye wangeweza kuingia ndani wala kutoka.
Katika msitari wa 2. Mungu ana mwambia Yoshua yakwamba, ameuweka Yeriko na vyote vilivyomo ndani mkononi mwake, lakini kuna KIZUIZI! Kwahivyo, lazima KIZUIZI kiondolewe ndiposa wana wa Israeli waingie ndani ya mji na wapate kuimiliki mji wa Yeriko pamoja na mazuri yote yaliyomo ndani yake.
Kwahivyo ilibidi walipe garama ya kuondoa kile kizuizi. Katika msitari ya 3; Mungu ana waamuru wana wa Israeli ili kuisunguka mji wa Yeriko mara mmoja kila siku kwa siku sita, kisha siku ya saba wausunguke mji mara saba, huku makuhani wakipiga tarumbeta yao ndipo ukuta ule ulio zuia mji utaanguka chini.
Swali ni kwamba, je kunayo kizuizi yeyote maishani mwako inayo zuia hatima yako?
AINA 4 YA VIZUIZI
1 DHAMBI;
Dhambi ni KIZUIZI inayo weka mipaka kati ya watu na Mungu. Mungu ni mtakatifu, kwahivyo hakuna usirikiano kati ya wenye dhambi na Mungu. kwahivyo dhambi ni KIZUIZI.
Biblia inasema katika kitabu cha ISAYA 59:1-2; Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweae kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; Lakini maovu yenu yamewafarakisha nanyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone , hata hataki kusikia.
Dhambi ni kizuizu, ambayo imetuzuia tusiuone uso wa BWANA, ukitaka BWANA asikie kilio chako, na maombi yako, lazima uondoe KIZUIZI wa dhambi ambayo umeuweka mipaka kati yako na Bwana.
< > METHALI 15:29; BWANA yu mbali na wasio haki; Bali huisikia sala ya mwenye haki.
< > ZABURI 34:15-16; Macho ya BWANA huwaelekea wenye haki, na masikio yake huielekea kilio chao. Uso wa BWANA ni juu ya watenda mabaya, aliondoe kumbukumbu lao duniani.
< > ISAYA 1:15-16; Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu. Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya.
Katika hayo mandiko, tuna jifunza ya kwamba BWANA wetu hasikii maombe ya wenye dhambi, hata waombe kwa maneno mengi, Mungu hasikii. kwahivyo lazima kwanza tuondoe KIZUIZI cha dhambi, ndipo BWANA atasikia maombi yetu. Na njia ya pekee ya kuondoa KIZUIZI wa Dhambi, ni toba. Ukitubu dhambi zako, na kumkiri YESU kuwa BWANA na Mwokozi wako, unaokolewa.
Mungu awabariki wote wenye watachukua nafasi yao kusoma ujumbe huu. Shallom, ngojea sehemu ya pili wa ujumbe huu wakati wowote. Shallom.