Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Tunapo sungumsia habari ya kufungiwa nira, tunaangalia katika Agano la kale.
Waamuzi 2:1-4; Tunaona hapa malaika wa Bwana aliwaamuru wana wa Israeli wasishirikiane na wenyeji wa nchi na wabomoe madhabau yao. Kubomoa madhabau ilimanisha kwamba wana wa Israeli wawafukuze watoke kwenye inchi lile. Mungu hakutaka wana wa Israeli wafungwe nira pamoja na wao.
Katika hilo kitabu cha Waamuzi 2:7 inasema; Watu hao wakamtumikia BWANA siku zote za Yoshua, na siku zote za hao wazee walioendelea siku zao baada ya Yoshua, hao waliyokuwa wameiona hiyo kazi kubwa ya BWANA yote, aliyokuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli.
Katika 2 Wakorintho 6:14-15 inasema:
14 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinzi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?
Kwenye hilo mandiko katika 2 Wakorintho 2:14-15, tunaonywa ili tusifungwe nira na wasioamini, maana hii ita adhiri uhusiano kati yetu na Mungu na hata waaminio. kama Wakristo tulio okoka, tukifungiwa nira na wasioamini, tutafanana na wao na matendo yetu itafanana na matendo yao, kwa sababu hiyo hatuta weza kuwaongoza katika njia za Kristo maana hatuta kuwa na uwezo ya kukemea matendo yao maovu.
1 Petro 3:15;
Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizae habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.
Wapendwa, tujitenge na uovu na kamwe tusijichanganye na waovu, bali tuwafundishe wasioamini uzuri wa kuokoka na kutembea na Kristo.
Mungu awabariki, tunapo tazamia siku ambayo Kristo atatoa hukumu wa haki kwa watu wote.