Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
1 Petero 5:5-6
5. Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam , nyinyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.
6. Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake.
Katika haya ya 5.ni dhahiri kwamba, Mungu hapendezwi na mwenye kiburi, ila uwapa wanyenyekevu neema. Mpendwa unasoma ujumbe huu, kuna tunda la unyenyekevu, ukinyenyekea, bwana wetu Yesu Kristo atakuinua.
katika msitari wa 6.inasema, nyenyekeeni. Neno unyenyekevu ni masharti kutoka kwa Mungu, kwamaana hapendezwi na mwenye kiburi. Mungu hushusha mwenye kiburi, na kuinua mnyenyekevu. Kwa hivyo ukitaka Mungu akuinue, ni lazima unyenyekee, chochote ufanyacho, fanya kwa unyenyekevu, sio kwa kiburi na masindano. YAKOBO 4:6; Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.
WAFILIPI 2:3; Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Mwenye kiburi hupenda kufanya vitu kwa masindano, anafanya hivyo ili apate kusifiwa na kujionyesha kwa sababu ya kiburi. Mungu hapendezwi na watu kama hawa, maana kiburi ni chukizo mbele ya Mungu.
METHALI 11:2; Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu. METHALI 16:18; Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko. METHALI 18:12; Kabla ya uharibifu moyo ya mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu. Kwa maneno mengine, tunda la unyenyekevu ni heshima, bali tunda la kiburi(majivuno) ni uharibifu(METHALI 29:23). METHALI 22:4; Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha bwana ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima.
REV. GEORGE ATANG'A