Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Biblia inasema katika kitabu cha Warumi 6:23
Kwa maana msahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katlika Yesu Kristo Bwana wetu.
Hakika dhambi linaleta mauti, na kumpokea Yesu utapata uzima, his ni kwa sababu; CHRISTO Yesu alikuja ulimwenguni, akafa kwa ajili ya kila mtu amwaminiye asifekatika dhambi, bali watubu dhambi zao na wapokee uzima. Ndiyo maana maandiko yasema katika kitabu cha Johana3:16; Kwa maana jinsi hii,Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele
Warumi 2:5 inasema; Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya basira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu.
Zekaria 1:3 inasema; Basi, uwambie BWANA wa majeshi asema hivi, nirudieni mimi asema BWANA wa majeshi, nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi
Ni wakati wa kugeuka na kutubu dhambi ,ili tumrudie BWANA Yesu, kwa moyo wetu wote, ndiposa Bwana pia, aweze kuturudia.