Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
AYUBU 1:1-22, 2:4-7
Leo hii nataka nisungumze juu ya kuweka tumaini letu kwa Yesu Kristo. Nataka kuangazia maisha yake Ayubu.
Ayubu alikua mcha Mungu aliye mkamilifu na mwelekevu, alikuwa na utajiri mkuu sana, alikuwa na kondoo elfu saba, Ngamia elfu tatu, Punda mia tano na jozi za Ng'ombe elfu tano. Alikuwa pia na wafanyikazi wengi. Hatahivyo, Ayubu alipitia mateso makali sana alipo jaribiwa na shetani.
AYUBU1:13-22; Ayubu alipotesa mali yake yote, lakini alisidi kuweka tumaini lake kwa Mungu. Alizingatia mambo ya ufalme wa Mungu kuliko mali ya dunia hii. Wapendwa mali ya dunia hii yana mwisho wake, hata uwe tajiri mkuu, utajiri wako unaweza kwisha ama ufe uziache, maana chochote kilicho na mwanzo, kina mwisho wake. METHALI 23:5
Ndiyo maana Paulo mitume kwenye barua yake kwa kanisa la Wakolosai 3:2 anawaambia; Yafikirini yaliyo juu, sio yaliyo katika nchi.
JOB 2:9 Mkewe Ayubu alikata tamaa akamwambia Ayubu amkufuru Mungu kisha afe, hata hivyo Ayubu alisimama imara kwa imani wala hakutoa tumaini lake kwa Mungu. Ijapo mkewe alijaribu kumshusha moyo, alisidi kuwa hodari wa imani. Job 2:12-13; Marafiki wake pia wakaja kumuona, badala wamtie moyo, wakasidisha machungu yake, kwakuwa walipofika maandiko yasema walipo mwona Ayubu kwa umbali, wasimtambue kwa sababu ya hali yake, badala wamuombee na kumtia moyo, walirarua mavazi yao, wakaanza kulia waka kaa pamoja naye mavumbini muda wa siku saba. kwa hayo yote Ayubu hakufa moyo, alizidi kuweka tumaini lake kwa Mungu.
Wapendwa wangu, msichoke kwa kutenda mema, maana hakuna hali ulioko wa kudumu, majaribio masito unayo yapitia sasa, yana mwisho wake. Mungu atakuondolea majario hayo na kurejesha yote yaliyo haribiwa na shetani. 1 Wakorintho 10:13
Mpendwa wangu, uenda umejawa na machungu moyoni kwa sababu ya yale unayopitia, uenda umepotesa ajira yako, labda ni biashara yako umefilisika, maisha yamekuwa magumu mno, mawazo yamekuzonga moyoni, uliyo wategemea wamekushusha moyo, ukiangalia mbele na nyuma hakuna msaada. Nataka nikutie moyo, msaada wako haupatikani kwa mwanadamu, msaada waku u katika Bwana wetu Yesu aliye mbinguni ZABURI 121:1-2.
Weka tumaini lako kwa Yesu aliye na uwezo wa kuondoa shida na dhiki unayopitia, Yesu ni mponyaji wa magonjwa yote ZABURI 147:3, YEREMIA 30:17, kwake hakuna jambo lisilowezekana, njoo kwa Yesu upate pumzikoMATHAYO 11:28, njoo kwa Yesu upate uzima, njoo kwa Yesu upate baraka WAFILIPI 4:19, njoo kwa Yesu upate uponyaji, njoo kwa Yesu akuondole mzigo msito ambayo umebebeshwa na shetani.
ahsanteni sana hata mnapo mchukuwa Kristo Yesu kuwa bwana na mwokozi wako.
Kasisi George Atang'a