https://www.mwokozi-wa-wote.org/uploads/source/audios/UTIMILIFU%20WA%20NDOTO%20YAKO.mp3Mithali 18:10 Jina la bwana ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.
Ulinzi wetu u mikononi mwa Mwenyezi Mungu, unapo mkimbilia,hatakuacha kamwe, maana yeye peke yake ndiye mchungaji mwema. Uwe na shida ya namna gani, ukimkimbilia, atalitatua mana hapana jambo lolote asiloliweza
Jee utamkimbiliaje kama hauja mpokea Yesu? Ndiyo maana nakusihi; mpokee Yesu, upate usalama.
MWENYEZI MUNGU NDIYE MLINZI WETU.
Huu ni habari njema kwa kila mmoja asikilizae unjumbe huu. Ukiwa ndani ya Yesu, na ukae kwa utakatifu, hakuna silaha zozote itakayo pangwa na maadui itakayo kupata, maana Mwenyezi Mungu atakulinda siku zote, popote uendako, macho ya Bwana utakuwa juu yako.
Katika biblia, kwa kitabu cha Zaburi 91:1-3 maandiko inasema; Aketiye mahali pa siri pake aliye juu, Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi. Msitari wa 2.inasema; Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumainia. Msitari wa 3. Maana yeye atakuokoa na mtego ya mwindaji, na katika tauni iharibuyo.
Katika Zaburi 23:4 biblia inasema, Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upo pamoja nami.Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
Menyezi Mungu ndiye mlinzi wetu, ukiwa hauja okoka, maisha yako himo hatarini, nakusihi leo, mpokee Yesu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako, maana bila Yesu hauna ulinzi tosha.
WIMBO WA KUABUDU MIMI NI MALI YA BWANA
KAZI YA ROHO MTAKATIFU KWA WATEULE
NENO LA UKOMBOZI
NYOTA YAKO ITANG'A
USICHOKE NGOJEA WAKATI WA MUNGU
TAFUTA BWANA MADAMU ANAPATIKANA