Kila mtu atendaye kazi upata thawabu, kwahivyo nasi tunayo tenda kazi katika mwili wa Kristo, kuna thawabu iliyo tayarishwa kwa ajili yetu. Chochote ufanyacho kwa ajili ya ufalme si bure, Mungu atakupa thawabu wakati wa Mungu ukifika.
Upako wa Roho Mtakatifu ni nguvu za kimungu ambayo mtu anapokea kutoka kwa Mungu kupitia Roho Mtakatifu. Ni uwezo na nguvu wa ndani unaotuwezesha kufanya kazi isiyo ya kawaida. Nguvu hii mtu upokea baada ya kupokea Roho Mtakatifu.