YOHANA 10:1114
Mimi ndimi mchungaji mwema, Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo
Mtu wa mshahara, wala si Mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia;na mbwa-mwitu huwakamata na kuwatawanya
Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara;wala mambo ya kondoo si kitu kwake.
Mimi ndimi mchungaji mwema;nao walio wangu nawajua;nao walio wangu wanijua mimi.
Zaburi 23:1-6
Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza. Kando ya Maji ya utulivu huniongoza.
Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za Haki Kwa ajili ya jina lake.
Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya; kwa maana wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.
Hakika wema na fadhili zitanifuata, Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele