Damu ni muhimu katika maisha ya mwanadamu, pasipo na damuya kutosha mwilini, hauwezi kuwa na uhai. Kwahivyo, damu ni muhimu katika maisha ya wanadamu, ila damu ya Yesu ni muhimu sana na ina nguvu.
Kuja kwake Yesu Kristo ulimwenguni mara ya kwanza, ilikuwa ni kwa njia ya kuzaliwa. Ijapo mimba ya Kristo Yesu haikuwa kwa uwezo wa mwanadamu, bali ilikuwa ni kupitia uwezo wa Roho Mtakatifu.