Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
WAGALATIA 3:9-4
9. Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani
10. Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye.
11. Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu mwente haki ataishi kwa imani.
12. Na torati haikuja kwa imani, bali, ayatendaye hayo ataishi katika hayo.
13. Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;
14. ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya amani.
Mitume Paulo anaita kazi ya sheria kuwa laana katika haya ya 10 kwa wale ambayo awasingati sheria na hawafuati sheria (Tasama pia Kumbu kumbu la torati 27:26). Msitari wa 13 inatwambia wasi wasi kwamba Kristo alitukomboa kutoka kwa laana ya sheria. Kwahivyo ikiwa Mungu mwokozi wetu Yesu Kristo, aliteswa na akafa msalabani ili tusiwe tena chini ya laana ya sheria.
Sikiza yaliyonenwa katika barasa ya Yerusalemu katika Matendo ya Mitume 15
MATENDO YA MITUME 15:5-11 inasema; 5. Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika torati ya Musa.
6. Mitume na wazee wakakusanyika wapate kulifikiri neno hilo.
7. Na baada ya hoja nyingi Petro akasimama, akawaambia, Ndugu zangu, ninyi mnajua ya kuwa tangu siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwenu ya kwamba mataifa walisikie neno la injili kwa kinywa changu, na kuliamini.
8. Na Mungu, ajuaye mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vile vile kama alivyotupa sisi;
9. wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani.
0. Basisasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua.
11. Bali twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao.
Katika msitari wa 10, Petro anauliza Wafarisayo waliyo amini sababu wana mweka Mungu katika majaribio ya maitaji (kuishi chini ya sheria) juu ya wayunani waaminiyo katika Yesu Kristo, maitaji ambayo wao wenyewe hawangwweza kusingatia.
Sisi hatuitajiki kamwe kuishi chini ya sheria leo. Sio hayo tu, bali hatuhistahili kujaribu hata kuishi chini ya sheria kwa sababu Biblia inasema yakwamba ni laana (Wagalatia 3:13). Na kwa ajili yake, hakuna mwili itakacho hesabiwa haki.(Warumi 3:20)
WARUMI 6:14 inasema; Sababu hiyo, dhambi haitakuwa bwana wako, maana hamuko chini ya sheria baali chini ya neema.
Endelea kutazamia juu
Kasisi George Atang'a