Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
MATENDO YA MITUME 2:17 Inasema; Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona MAONO; na wazee wenu wataota ndoto.
kwenye huo mandiko katika Matendo ya Mitume, ina tufundisha kuelewa kwamba, MAONO hupatikana kama matokeo wa Roho Mtakatifu, na bila kujazwa Roho Mtakatifu, ni vigumu kupata maono. Ndiyo maana Luka anaandika ujumbe huo kwa kitabu cha Matendo Ya Mitume akimaanisha sauti ya naabi Joeli 2:28.
METHALI 29:18; Pasipo maono, watu huacha kujizuia; bali ana heri mtu yule aishikaye sheria. Kwa tafsiri ya kimombo inaitoa kwa uzito; inasema pasipo maono, watu huangamia.
Mungu hawezi kupa kitu kile auoni, unapo piga magoti nakuomba, ni vema uwe na picha ya kile unaitaji ama uwe umeiona kwa macho yako ya rohoni kile unacho omba Mungu akutende. Kama ni nyumba, unafaa kuwa na picha ya aina ya nyumba unachoitaji, kama ni kazi vilwvile upate picha ya kazi ambayo hata ukienda katika magoti yako kwa maombi, unaweza kumwonyesha Mungu
Daudi anasema katika kitabu cha ZABURI 119:18; Unifumbue macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako .
HABAKUK 2:2-3; Bwana akanijibu, akasema, andika jonzi(MAONO) ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. 3.Maana jonzi(MAONO) hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.
WAEFESO 1:18; Macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwiyo wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo.
Thanks you so much and please keep on looking above