Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
WAEFESO 1:13 inasema:
Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.
Mungu amefanya jambo lisilo la kawaida na la miujiza. Ameliweka Roho Mtakatifu ndani ya kila muumini katika Kristo Yesu, na Mungu ametutia muhuri na huyo Roho. Je haikutosha ya kuwa Christo Yesu alikufa juu ya msalaba? Je haikutosha yakuwa Christo Yesu baada ya kufa, alizikwa kaburini siku ya tatu akafufuka kutoka kwa waafu? Je tukiisha amini hayo ya tosha? la sivyo, Baada ya kuamini, tunapaswa kujashwa Roho Mtakatifu kama muhuri wa dhibitisho ya kwamba tumefanyika wana wa Mungu(MATENDO YA MITUME 2:4)
Mungu ametupa wokovu mkuu, lakini hayo hayakutosha, baada ya kuokoka anatupatia vipawa vya Roho Mtakatifu.
2 WAKORINTHO 13:12 inasema;
Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu wayahudi , ou kwamba tu wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.
1 WAKORINTHO 3:16 inasema;
Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
ROHO MTAKATIFU KATIKA AGANO LA KALE KAMA CHANZO CHA UHAI
Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindivya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji(MWANZO 1:2)
Roho ya Mungu imeniumba, na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai(AYUBU 33:4)
Waipeleka roho yako, wanaumbwa, nawe waufanya upya uso wa nchi(ZABURI 104:30)
ROHO MTAKATIFU KAMA MWALIMU NA MWONGOZO
Ukawapa na roho yako mwema ili kuwaelimisha, wala hukuwanyima mana vinywani mwao, tena ukawapa maji kwa ajili ya kiu yao(NEHEMIA 9:20)
KATIKA AGANO LA KALE, ROHO MTAKATIFU ILIKUJA JUU YA WATU
Ndipo Samsoni na baba yake na mama yake wakatelemkia Timna, wakafika mashamba ya mizabibu huko Timna; na tazama, mwana-Simba akamngurumia. 6. Roho ya Bwana ikamjilia kwa nguvu, naye akampasua kana kwamba anampasua mwana-mbuzi, wala hakuwa na kitu cho chote mkononi mwake; lakini hakuwaambia baba yake na mama yake aliyoyafanya(WAAMUZI 14:5-6)
KATIKA AGANO LA KALE ROHO YA MUNGU HAIKUWA WA KUDUMU JUU YA WATU
Usinitenge na uso wako, wala Roho yako mtakatifu usiniondolee(ZABURI 51:11)
Mmoja ya kusudi ya kuweka muhuri wa Roho Mtakatifu kwa waumini wa agano jipya, ni hakikisho kwamba Roho Mtakatifu haita ondoka ndani yao. Atasalia milele ndani ya wote waaminio injili ya Christo Yesu iletao wokuvu na anatupatia hakikizo(1 WAKORINTHO 15-1-4)
WAEFESO 1:14 inasema;
Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake
WAFILIPI 1:6 inasema;
Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu
Hatimae WARUMI 8:38-39 inasema;
Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.
ENDELEA KUTAZAMIA KURUDI KWAKE YESU
MUNGU AWABARIKI
REV GEORGE ATANG'A