Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Katika biblia kwa kitabu cha WARUMI 3:5, Paulo ana weka wasi wasi kwamba kuhesabiwa haki na MUNGU inatokana na imani katika KRISTO pekee. Hi ndiyo njia pekee mwanadamu uokolewa. Nina amini kutoka kwa WARUMI 6 kwendelea mbele Paulo anafundisha waumini katika KRISTO njia pekee ya kushinda miili yetu na kuishi maisha ya Ukiristo ni kwa kutiwa upya mawazo yetu. Sasa hatuongozwi kwa sheria ya dhambi na kifo, ila sasa tunaongozwa kwa sheria ya Roho wa uzima katika KRISTO YESU (WARUMI 8, 2WAKORINTHO 3). Hili linawezekana tu kwa wale ambayo tayari wameokoka kwa kuamini KRISTO pekee anaye samehee dhambi. (WARUMI 3:19-28, 4:5, 5:17-19).
Kuna mambo ambayo lazima tuhesabu kwa maisha ya mwili huu inayo kufa kama waumini ili tubadilishwe katika maisha hii tunayoishi. Paulo anafundisha waumini kwamba tulibatiswa katika kifo chake YESU KRISTO ambayo inamanisa kwa Roho kwamba tulifanywa kuwa hai katika kazi ya Roho Mtakatifu. Kupitia kazi hii,muumini anafanywa kuwa mfu katika dhambi, lakini kuwa hai kwa MUNGU (WARUMI 6:2-3, 8-11)
Sisi kama waumini tunaunganishwa pamoja naye kwa Roho, na ndani yake hamna dhambi (1 WAKO.6:17, 1JOHN 3:5). KRISTO ndiye utimilifu wa sheria kwa wale wameunganishwa naye kiroho, na sasa hatuko tena chini ya sheria (JOHANA 7:4-6), Mahali hapana sheria, hamna dhambi (WARUMI 5:13-15, 1 JOHN 3:3-5)
Tunafanywa kuwa wakamilifu katika mmoja kupitia ubatizo wa kiroho na miili yetu inahesabiwa kufa kwa sababu ya dhambi, lakini Roho ni uhai kwa sababu ya haki.(JOHN 17:23, ROMANS 8:10)
Haya ndiyo ukweli wa maandiko ambayo muumini anapaswa kupokea na kufikiria kila siku ili kubadilishwa katika maisha haya na MUNGU. Paulo analiita, kutembea kwa Roho(WARUMI 8:4-5). Kuwa na mawazo ya kimwili ni kuamini ya kwamba sheria inaweza kutuongoza katika njia za haki, ila tunapata ya kwamba sheria uwaziri tu wa kifo kwa kuwa ni nguvu ya dhambi. Waumini lazima waongozwe kwa Roho ambayo ni uwaziri wa haki (WARUMI 8:6, 1 WAKORINTHO 15:56, 2 WAKORINTHO 3:6-11)
ASANTE SANA NA TUENDELE KUTASAMIA KRISTO YESU