Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Wafilipi 2:19-21 inasema;
19. Walakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo afike kwenu karibu, nifarijiwe na mimi nikiijua hali yenu.
20.Maana sina mtu mwingine mwenye nia moja nami, atakayeiangalia hali yenu kweli kweli.
21. Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Kristo Yesu
Tunapo soma neno la Mungu, ni vizuri kukumbuka ya kwamba watu kama Paulo, Petero na Yohana hawakukabiliwa na majaribio ya kutoka inje, baali walikabiliana na majaribio kutoka kwa wandani wao. Kulikuwa na waumini ambayo hawakuitaji vitu vya Mungu, bali walifanya Paulo afanye kazi ya Mungu kwa ugumu sana.
Mojawapo ya mtu wa maana aliye muacha Paulo alikuwa anaitwa Demas. Demas alikuwa na Paulo kule mji wa Roma.
Wakolosai 4;14-16 Paulo anawatia moyo waumini iakisema:
14. Luka, yule tabibu mpendwa, na Dema wanawasalimu. 15. Wasalimuni ndugu walioko Laodikia, na nimfa, na kanisa lililo katika nyumba yake. 16. Waraka huu ukiisha kusomwa kwenu fanyeni kwamba usomwe katika kanisa la Walaodikia pia; na ule wa Laodikia usomwe na ninyi.
Baadaye, Demas akamwacha Paulo. Na hiyo Paulo amelitaja katika 2 Timotheo 4:10; Maana Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu huu wa sasa, akasafiri kwenda Thesalonike ; Kreske amekwenda Galatia; Tito amekwenda Dalmatia.
1 Timotheo 6:12 inatuambia yakwamba;
Piga vita vile vizuri vya imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi.
Waefeso 6:10-11 inasema;
Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 11. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani
Wagalatia 6:10 inasema;
Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.
Waumini katika Kristo Yesu watapitia hali mgumu na kushushwa moyo kwasababu ya waumini wengine na wasiyo amini, lakini tusivunjike moyo- Lile neno la Mungu alilonena Paulo bado linasalia moyoni mwetu.
Wafilipi 1:6 ambayo inasema;
Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu.
Asanteni sana, na tuendele kutasamia kurudi kwake Yesu Kristo