Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Waumini wengi hata baada ya kuokoka, bado wana tabia ya kiutoto na ukisikia jinzi wanapo ongea ama ukiona tabia yao kwa jumla, unagundua ya kuwa baado hawajakoma kiroho.
Paulo mitume ana nena na kanisa la Wakorintho katika barua yake kwenye kitabu cha; "1WAKORINTHO 13:11; Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyapatilisha mambo ya kitoto".
1 WAKORINTHO 14:20 >Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu; lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga bali katika akili zenu mkawe watu wazima.
HATUA YA KWANZA NI "WOKOVU"
Wokovu ni kuzaliwa mara ya pili ama kumpokea Kristo Yesu kuwa bwana na mwokozi wetu. YOHANA 3:3; Yesu akajibu, akamwambia, Amin amin, nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuona ufalme wa Mungu.
HATUA YA PILI NI "UKOMBOZI" Kuna wakristo wengi ambayo wameokoka, lakini baado wako katika kifungo cha adui, wengine wameokoka na wana kiri bwana asifiwe, lakini bado wako katika kifungo cha ulevi, wengine tama ya mwili, wengine ni ufisadi na kadhalika. Paulo mitume kwa barua yake katika "2WAKORINTHO 5:17; Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! yamekuwa mapya.
WAEFESO 4:31; Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya.
HATUA YA TATU "UBATIZO"
Ubatizo ni ishara ya kufa na kufufuka na Kristo, kila muumini baada ya kuokoka ni sharti abatizwe katika maji mengi
YOHANA 3:5; Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu.
MATENDO YA MITUME 2:38; Petro akamwaambia , Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho mtakatifu.
HATUA YA NNE "KUJAZWA ROHO MTAKATIFU"
Baada ya kuoka na kubatizwa, unafa kupokea Roho Mtakatifu, kwakuwa tunaongozwa na Koho Mtakatifu
1WAKORINTHO 6:19; Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu, bali nyinyi si mali yenu mwenywewe.
YOELI 2:28; Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina Roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono.
HATUA YA TANO "MAJARIBU"
Majaribu ni hali yakujaribiwa ili kubaini ukomavu ya kiroho, AYUBU 23:10; Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.
YAKOBO 1:2-4; Ndugu zangu, hesabuni yakuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; Mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.
Tukisingatia hatua hayo matano, tutafikia hatua ya ukomavu ya kiroho, wala hatuta tingizwa na jambo lolote.
ENDELEA KUTAZAMIA KRISTO YESU.