Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Ni Roho Mtakatifu anaye tuwezesha kufanya kazi katika uduma wa Yesu Kristo. Ndio mana kabla Yesu kuondoka duniani, aliwashauri wanafunzi wake ili wasiondoke Yerusalemu mpaka Roho Mtakatifu adhihirishwe. "MATENDO YA MITUME 1:4; Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu." LUKA 24:49; Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini , hata mvikwe uwezo utokao juu.
MATENDO YA MITUME 1"8; Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
< > ROHO MTAKATIFU NDIYE CHANZO CHA "HEKIMA"
Kwa kila kazi tufanyayo, iwe ni ya huduma katika mwili wa Yesu Kristo, ama katika jamii, ama mahali pako pa ajira ama biashara, unahitaji hekima. Sasa ni Roho Mtakatifu anaye tupatia huo hekima itokayo kwa Mungu.
YAKOBO 1:5; Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu wala hakemei; naye atapewa.
WAEFESO 1:17; Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi Roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye.
<> ROHO MTAKATIFU NDIYE CHANZO CHA "UFUNU
1 WAKORINTHO 2:10-11; Lakini Mungu ametufunulia sis kwa Roho. Maana Roho uchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.
YOELI 2:28; Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu yao wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono.
< > ROHO MTAKATIFU NDIYE CHANZO CHA "NGUVU"
1 SAMUELI 10:6; Na Roho ya Bwana itakujilia kwa nguvu, nawe utatabiri pamoja nao, nawe utageuzwa kuwa mtu mwingine.
MATENDO YA MITUME 1"8; Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
< > ROHO MTAKATIFU ANATUSAIDIA KWA "O"MAOMBI"
WARUMI 8:26; Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkua.
< > ROHO MTAKATIFU ANATUSAIDIA KUELEWA "MAANDIKO MATAKATIFU"
LUKA 24:45; Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.
YOHANA 14:26; Lakini huyo msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
< > ROHO MTAKATIFU ANATUSAIDIA KUISHI MAISHA "MATAKATIFU"
WAGALATIA 5:16; Basi nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtatimiza kamwe taama za mwili.
< > ROHO MTAKATIFU ANATUSAIDIA KWA "MAABUDU"
YOHANA 4:24; Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye, imewapasa kumwabudu katika Roho nakweli.