Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
IMANI kulingana na mwaandishi wa bibiloia katika kitabu cha "Waibrania 11:1; Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana."
Kwahivyo, kuishi maisha ya imani ni kuishi maisha kuwa na hakikisho ya ushindi, mtu wa imani hafunjiki moyo, hata kama jambo limechelewa, bado tu angali na hakikisho yakwamba itatimia.
Imani ni macho ya kiroho ya ndani yanayoona mambo ambayo macho ya kimwili hayawezi kuyaona.
Waibrania 11:8; Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa uridhi; akatoka asijue aendako. Ibrahimu aliitwa baba ya imani maana alitenda mambo yake kwa imani, wala si kwa kuona kwa macho huu wa kimwili. Hapa tuaona Mungu anamuamuru Ibrahimu atoke, aache boma ya babake, na urithi wote na watu wa kwao, na aende mpaka mahali atakapo ambiwa na Mungu. Naye Ibrahimu akaheshimu sauti ya Mungu nakuondoka kwa imani asijue anaelekea wapi; atakaa namna gani na atakaa wapi. hiyo ni imani kuu lisilo na mashaka.
2 Wakorintho 5:7; Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.
Waibrania 11:6; Lakini pasipo imani, haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
wapendwa atuwezi kumpendeza Mungu kama hatuna imani. Hata kama umeombewa juu ya uponyaji, na hauja aamini moyoni kwamba umepona, maombi hayo hayata kusaidia kwamaana uko na shaka. Mtu kama huyo hampendezi Mungu, na pasipo kumpendeza Mwenyezi Mungu, hawezi kuyajibu maombi yako. Katitaka biblia kwa kitabu cha Mariko 5:25-29, tunasoma historia ya mwanamke aliye tokwa na damu kipindi cha mwaka kumi na miwili, alipo mwendea Yesu akiamini moyoni mwake kwamba hata akiguza tu pindo la vasi ya Yesu, atapona. Imani ya huyu mwanamke ili fanya damu ikawke baada ya kipindi kirefu ya matezo. Nasi vile vile tukiomba chochote tukiwa na imani, tutapata. "Mariko 11:24; kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu".
Kwa maombi ya imani, Hanah mkewe Elkana alichukuwa mimba baada ya miaka nyingi ya utasa, akazaa mtoto mwanaume, akamwita jina lake Samueli.(1 Samuel 1:12-18)
Kwa imani, Shadrak, Meshak na Abednego waligeuza amri ya mfalme (Daniel 3:16-30)
Waefeso 6:16; Zaidi ya yote mkitua ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
Endelea kuwa na imani kwa chochote utakacho kwa Mungu, nakuomba maombi ya imani