Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Neno la Mungu liko na nguvu na uwezo, bila huo Neno hakuna chochote kilicho ambayo lingekuepo, vitu vyote vilivyomo ulumwenguni kiliumbwa kwa neno; Wanyama porini, Samaki baharini na Ndege za angani, wote waliumbwa na Mwenyezi Mungu kupitia Neno. Hata ilipowadia wakati wa kuumba mwana adamu, ijapo ilikuwa wa tofauti na viumbe vingine, lakini neno ilitamkwa; "MWANZO 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu" Mungu aka sungumza.
Kwahivyo Neno la Mungu lina uwezo wa kuumba, kuleta uhai na kufanya kitu kisicho na kiwepo.
YOHANA 1:1 Inasema; Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Kwenye mtasamo wa hii ukurasa wa Yohana, tunajifunza jambo, Neno ilikuwa ni Mungu, inamanisha ya kuwa hili neno ninayo waletea siyo matamshi , bali ni utu. Sasa suali ambayo watu ujiuliza ni, huyu neno aliyetoka kwa Mungu, naye alikuwa ni Mungu na vitu vyote vilifanyika kwake ni nani?
YOHANA 1:14; Naye neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu kama wa Mwana pekee atokae kwa Baba; amejaa neema kwa kweli. Sasa kwa Yohana 1:14 inahihirisha kwamba Neno ni KristoYesu, aliyekwepo hapo mwanzo kabla ulimwengu kuumbwa, akawa pamoja na Mungu.
MATHAYO 4:4 Naye akajibu akasema, imeandikwa, mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa neno litokalo katika kinywa cha Mungu. Hi inamanisha ya kwamba YESU ndiye neno, na hatuwezi kuishi bila Kristo Yesu ambaye ndiye Neno. Kwahivyo kama mtu hajampokea Kristo kuwa bwana wa maisha yake, maisha yake kiko hatarini. MITHALI 30:5 Kila neno la Mungu limehakikishwa, yeye ningao yao wamwaminio.
Neno la Mungu ni uzima, Neno la Mungu ndiye ngao letu, neno la Mungu ni Amani, Neno la Mungu ni uponyaji, kwa Neno hilo vipofu wanaponya, kwa neno hili Mujisa mbalimbali
kwahinyo tafadhali, kama ujampokea Kristo Yesu, hu ndiyo nafasi yako.