Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Wapendwa sisi ndie silaha za vita mkononi mwa Mungu.Tunapo soma kwenye maandiko katika kitabu kitakatifu cha YEREMIA 51:20-24 Mungu anasungumza na nabi Yeremia akimwambia jinzi atakaye mtumikia kama silaha mkononi mwake; katika msitari wa 20. "Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitavunja - vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme".
Silaha haina uwezo wa kufanya chochote, mpaka mwenyewe ndiye aamuwe jinzi anavyotaka silaha lifanye kazi. Vilevile nasi kama silaha za Kristo, hatuna uwezo wa kufanya chochote pasipo nguvu na uwezo wa Mwenyezi Mungu kupitia Roho Mtakatifu. Sisi ni vyombo tu, hatuna uwezo wa kukemea hata shetani na aweze kutii, ila tukifanya hivyo katika jina la Yesu Kristo, ata tii nakuondoka, hivyo basi silaha haina nguvu, ila tu kwa uwezo na nguvu ya mmiliki wake. Ukiomba mgonjwa apone, sio wewe ni Kristo maana wewe hauna nguvu ya kuponya mgonjwa,ila ni mmiliki wako ambaye ni Kristo, kama vile imenakiliwa kwa "WAGALATIA2:20 Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu"; Unapo toa unabi na itimilike, sio wewe, wewe ni chombo tu ya kunena, ila aanayekupa ya kuzungumza yu ndani yako, ni Kristo Yesu kupitia Roho Wake Mtakatifu, usijivunie yakuwa ulitoa unabii na ikafanyika jinzi ulivyonena, hapana si wewe ni Mungu ambaye ndiye mmiliki wa silaha. ISAYA 10:15; Je! Shoka lijisifu juu yake alitumiaye? Je! Msumeno ujitukuze juu yake autumiaye? Ingelikuwa kana kwamba bakora ingewatikisa waiinuao, au fimbo ingemwinua yeye ambaye si mti.
Nikiwa na Yesu Kristo, hakuna jambo sitaweza kuyafanya, kwa kuwa sio mimi niifanyaye, bali ni Kristo aishiye ndani yangu. Kwahivyo mimi sina jambo lolote la kujivunia, ila chochote nifanyacho na kufaulu, sifa na utukufu inamrudia Mungu, nikifaulu kupata ndoa, sifa ni kwa Yesu, nikifaulu kupata kazi, sifa na utukufu ni kwa Yesu, nikifaulu masomo, sifa kwa Yesu, nikipata mtoto kwenye ndoa yangu, sifa na utukufu kwa Kristo Yesu, Maana si kwa nguvu zangu wala kwa uwezo wangu, baali ni kwa uweza wa Bwana wangu Yesu Kristo aliye ni wezesha. Hakika sisi ni silaha tuu mkononi mwa Yesu Kristo. WAFILIPI 4:13; "Nayaweza mambo yote katika Yeye anitiaye nguvu"
Daudi alikuwa silaha mkononi mwa Mwenyezi Mungu alipo mwaangusha mfilisti aliye kuwa na majivuno mengi na kuwatusi wana wa Israeli. Daudi akamwambia huyo mfilisti, wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana. 1 SAMUELI 17:45-46
Musa akawa silaha mkononi mwa Mwenyezi Mungu, Mungu akamtumikia kukomboa wana wa Israeli kutoka utumwani kule misri. Na wengine wengi tunayo soma kuwahusu ndani ya biblia.
Je leo hii, u tayari kufanyika silaha mkononi mwa Mungu?
1. Lazima uokoke ili Yesu adumu ndani yako
2. Lazima uwe mnyenyekevu, maana Mungu anawatumikia walio na moyo wa unyenyekevu
3. Unapasua kujaa Roho Mtakatifu
4. Mungu anapokutumia kwa eneo lolote, usijitualie utukuvu