Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Daudi amenakili ujumbe katika kitabu cha Zaburi 91 kuhuzu umuhimu wa kuka katika uwepo wa Mwenyezi Mungu. Katika msitari wa kwanza maandiko inasema; 1. "Aketiye mahali pa siri pake aliye juu Ataka katika uvuli wake Mwenyezi". Uvuli ni uwepo wa mwenyezi, kwahivyo ukisikia Daudi akisema kuhusu kuka katika uvuli, anamaaniza kudumu katika uwepo wa Mungu
Msitari wa pili anasema; 2. Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini. Yani, katika uwepo wa Mungu kuna usalama, kuna uponyaji, kuna baraka na vyote tunavyohitaji.
Isaya mnaabi pia anatuhimiza kuwa na ujasiri tukiwa uweponi pa Mwenyezi
Isaya 41:10; Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
Musa akiwatoa wana wa Israeli katika utumwa, kabla aanze safari, Musa akamwambia Mwenyezi; kama hauta enenda nazi, usitutoe hapa, naye Mungu akamwambia Musa; uwepo wangu utaenenda pamoja nanyi. Kwahivyo, Musa pamoja na wana wa Israeli, walikaa katika uwepo wa Mwenyezi. Je wewe usomae nakala hiki, tafadhali kama ujapokea Kristo, tafadhali tafuta Mungu akuokoe ili ukaweze kuka na kudumu katika uwepo wa Roho mtakatifu.
Kumbu kumbu 31:8; Naye Bwana, yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja, hatakupung wala kukuacha.; usiogope wala usifadhaike.
Nataka kunena pointi tatu;
1.Katika uwepo wake kuna usalama; Zaburi 31:20 Utawasitiri na fitina za watu katika sitara ya kuwapo kwako; utawaficha katika hema na masindano ya ndimi. Zaburi 91:4; kwa manyoya yake atakufunika Chini ya mbaya zake utapata kimbilio uaminifu wake ni ngao na kigao. Katika Zaburi 23:4; Naam, nijapopita kati ya bonde la uvule ya mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upowewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.