Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
1 WAKORINTHO 15:1-4; Basi, ndugu zangu, nawaarifu ile injili niliyowahubiri; ambayo ndiyo mliyoipokea , na katika hiyo mnasimama. na kwa hiyo mnaokolewa ; ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiri isipokuwa mliamini bure. Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na y akuwa alizikwa ; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko.
YOHANA 10:27-30; Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya mkononi mwa Baba yangu.Mimi na Baba tu umoja.
ROMANS 8:31-32; Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwa upande wetu, ni nani aliye juu yetu? Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, baali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?
1 WAKORINTHO 1:8 Inasema: Ambaye atawadhibitisha hata mwisho , ili msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.
WAEFESO 1:3-4; Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa msingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.
Katika WAEFESO 1:13-14 INASEMA; Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli , habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.
Kwa hayo yote, tuna hakikisho la wokovu wetu katika Kristo bwana wetu. Kwahivyo mpendwa wangu ikiwa umeamini neno hili tunalo ubiri nakukiri dhambi zako, Bwana wetu Yesu Kristo atakusamehe, na utapata wokovo.
1 PETERO 1:3-5; Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu; tupate na uridhi usioharibika,usiyo na uchafu, usionyauka, uliotunzwa Mbinguni kwa ajili yenu. Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.
Endelea kutazamia juu mbinguni, aketiye Bwana wetu Yesu Kristo katika mkono wa kuume wa Mungu Baba.
Rev. George Atang'a