Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Hofu na wasiwasi huondoa imani katika maisha ya waumini.
Kulingana na mwandishi wa kitabu cha Waebrania 11:1 anasema; Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Lakini shetani anapoweka hofu na wasiwasi ndani yako, ataondoa imani ndani yako na kuweka mashaka. Na ukiwa na mashaka, hataukiomba mara ngapi, Mungu hawezi kuyajibu maombi yako maana Mungu hapendezwi na wenye mashaka. Kwa hivyo wapendwa, usimruhusu shetani kuweka woga na mashaka ndani yako. Ukiomba uwe na imani pasipo na shaka, kwamba Mungu atayajibu maombi yako.
Katika mandiko, kitabu cha Isaya 35:4, inasema; Waambieni walio na moyo wa hofu, Jipeni moyo, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja na kisasi, na malipo ya Mungu. Atakuja na kuwaokoa ninyi.
Zaburi 23:4, inasema; Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya; kwa maana wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
Tukiwa na Kristo Yesu, hatuta ogopa wala kuwa na hofu kwa chochote, maana yeye Bwana upo pamoja nasi. kwahivyo mpendwa, ukiomba, uwe na imani ya kwamba Bwana atajibu na kukutendea unayo yaitaji. Usimuruhusu shetani atie shaka ndani yako, hata kama unapitia hali mgumu namna gani, usiingiliwe na hofu, msubiri bwana, tajibu maombi yako
2Timotheo 1:7 inasema; Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi
Mpendwa, mtumainie Mungu wala usi hofu moyoni mwako kwa sababu ya yale mambo unayapitia, bali jivike imani nakuendelea na maombi ya imani. Maana Mungu hajatupa roho ya woga. Zaburi 125:1, inasema; Wamtumainio BWANA ni kama milima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele.
Tukiweka matumaini yetu kwa Kristo Yesu, hatuta tikisishwa na jambo lolote, vita viinuke kinyume chetu, hatutaogopa; Magonjwa yaje, haita tutikisisha; shida ije tuta simama imara katika Yesu, wala hatuta ogopa. Mpenwa wangu, ondoa hofu na wasiwasi moyoni mwako, amini Mungu ya kwamba, chochote unacho pitia, sio ya kudumu, bali itakuja kupita.
by Bramwel were// Zilizowekwa 09 Agosti 2021// Bendera kama haifai // Jibu // Ghairi jibu
by Rev George Atang'a// Zilizowekwa 14 Agosti 2021// Bendera kama haifai // Jibu // Ghairi jibu