Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
ZABURI 23:1-4
hili ni Zaburi ya Daudi, maandiko yasema; Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. Katika Malisho ya majani mabichi hunilaza. Kando ya Maji ya utulivu huniongoza. Hakika tukiwa na bwana Yesu, hatuwezi kupungukiwa nakitu Maana anavyo viote tunavyo vihitaji.
Tukiwa na mchungaji Kristo Yesu, hatutaogopa chochote, Maana yu pamoja nasi, popote tuendako yu pamoja nasi, kama vile maandiko yasema katika Zaburi 23:4; Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya; kwa maana wewe upo pamoja nami. Gongo lako na fimbo yako vyanifariji. Hatutaogopa mabaya, hatutaogopa maadui, hatutaogopa magonjwa, Maana anaye tuchunga halali wala hasinzi.
Katika kitabu cha YOHANA10:11,maandiko inasema; Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. Hakika Yesu ni mchungaji mwema, alitoa uhai wake ili sisi zote tusipotee, bali tuweze kuokolewa ,kutoka kwenye kifungo cha dhambi. ZABURI 28:9, inasema; Uwaokowe watu wako, uubariki uridhi wako. Uwachunge, uwachukuwe milele. Kristo Yesu ndiye mchungaji wetu na sisi ni uridhi wake. Leo hii nina habari njema , njoo kwa Yesu awe mchungaji wako, hakuna ajaye kwake amemtupa. Ukimfanya Yesu awe mchungaji wako; Yeye atakuokoa na maovu, atakuchunga kinyume na maadui wako, atakuchunga kinyume na magonjwa yasiyo na tiba, atakufunika kwa mabawa yake, hakika utakuwa salama. Njoo kwa Yesu umpokee awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Ukisikia habari hili, usifanye moyo wako kuwa mgumu.