Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
MATHAYO 28:1-11
1.Hata Sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.
MATHAYO 28:2; "ufufuo wa Yesu ilikuwa ya nguvu mno, na kusababisha tetemeko la nchi". Walipomuua wakadhania wame mumaliza, wakachukua jiwe kubwa wakaweka kwenye lango la kaburi lake. Lakini ilipowadie siku ya tatu kama vile alivyo tabiri; MARIKO 9:31 - Kwa sababu alikuwa akiwafundisha wanafunziwake, akawaambia, mwana wa Adamu yuaenda kutiwa katika mikono ya watu, nao watamua; hata akiisha kuuawa, baada ya siku tatu atafufuka.
Kifo na ufufuo wa KRISTO YESU, ina umuimu sana katika maisha yetu, ama kwa hakika ni kwa sababu yetu ili tuokolewe na kukombolewa kwa damu yake. Paulo Mitume amenakili kwenye barua yake kwa Wafilipi kuhusu nguvu ya ufufuo. WAFILIPI 3:10; Ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake.
Mungu baba alimtoa Yesu mwanaye kama kafara ya ondoleo la dhambi, alitezwa kwa ajili yetu, kama vile Isaya mnabi anavyo sema kwenye kitabu cha ISAYA 53:4-5; Hakika ameyachukuwa masikitiko yetu, Amejitwika huzuni yetu; lakini tulidhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
YESU alilipa garama ya ukombozi wetu, aliteswa kwa ajili yetu, aliwawa kwa ajili yetu, aliyabeba laana yetu juu yake kule msalabani. Kwa hivyo garama yote aliyalipa kupitia kifo chake, ndiposa YESU alisema, Yote yamekwisha. Kama YESU alikulipia garama, mbona bado wafanya dhambi? mbona bado watembea katika laana? Mbona magonjwa bado yana kutiza ilhali mandiko yasema kwa kupigwa kwake sisi tumepona, leo hii ukitaka kifo cha YESU iwe na maana kwako lazima utatubu.
1 PETERO 1:3; Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu.
WAEFESO 2:6; Ametufufua pamoja naye, akatuketisa pamoja naye katika ulimwengu wa Roho, Katika Christo YESU.
WAKOLOSAI 3:1; Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, Yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko Kristo aliko. ameketi mkono wa kiume ya Mungu.
WAGALATIA 2:20; Nimesulubiwa pamoja na KRISTO; lakini ni hai; wala si mimi tena bali Kristo yu hai ndani yangu, na uhai niliyo naosasa katika mwili, nonao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.
2 WAKORINTHO 5:15; Tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe haitena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao.
Asante, endelea kutazamia juu mahali aketiye Kristo katika mkono wa kuume wa Mungu baba akituombea sisi watoto wake kila siku, na kama haujaokolewa, tafadhali okoka ili uwe mwana wa Mungu.