Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Mara kwa mara tunapo songea mbele za Mungu kwa maombi, watu wengi usahau kutangulisa Toba kabla ya kuendelea na maitaji mengine. Kama mwana damu, kuna uwezekano kumkosea Mungu kwa njia mmoja ama nyingine, kwa kujua ama kwa kutojua, lakini kwa haya yote, dhambi ni chukizo mbele za Mwenyezi Mungu, na Mungu hazikii maombi ya mwenye dhambi. So ndiyo maana nakushauri mpendwa, ukiwa mbele za Mwenyezi Mungu kwa maombi, jifunze utaratibu ya kuanza maombi kwa kutubu. Maandiko inasema kwa kitabu cha 1 Yohana 1:8; "Tukisema kwamba hatuna dhambi,twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu".
Kwanza anza na toba, kisha baada ya toba ni maombi ya shukrani, kumshukuru Mungu kwa yale amekutendea, kisha unaweza kuwasilisha ombi la mambo mapya ambayo ungelipenda Mungu akutendee.
2 Chronicles 7:14; Ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya inchi yao.
Kutokana na maandiko hayo kwenye Kitabu cha Mambo ya Nyakati wa pili, tuna jifunza umuhimu wa Toba, ndiyo maana inasema, watu wangu walioitwa kwa jina langu. Watu walioitwa kwa jina la Mungu ni watoto wa Mungu; yaani watu walio okoka. Kama vile maandiko yasema katika kitabu cha "Yohana 1:12; Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake". Naye katika haya ya 15 katika kitabu cha Mambo ya nyakati 7:15; "Sasa macho yangu yatafumbuka, na maskio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa". Hii ni baada ya kutubu.
Maubiri ya Toba ilianzishwa na KRISTO mwenyewe, na hata sasa, tuna tangaza ujumbe wa Toba. Mathayo 4:17; Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa Mbinguni umekaribia.
Matendo ya mitume 17:30; Basi, zamani zile za ujinga, Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wan kila mahali Watubu.
Toba ni lazima kwa kila mtu, uwe haujaokoka, lazima utubu dhambi zako na uokolewe, uwe umeokoka, jioji kama kuna vile umefanya jambo lisilofa machoni pa Mungu, Tubu. Maana Mungu wetu anasikia kilio cha wenye haki, ukiwa na dhambi moyoni ama umetenda tendo la dhi, Mungu hawezi kuyajibu maombi yaki, maana maombi ya mwenye dhambi ni kelele maskioni mwa Mungu, isipokuwa uki Tubu, atasikia na kuyajibu maombi yako.
Endelea kutafuta uso wa Bwana kwa toba na maombi.