Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Kwanini YESU alikuja ulimwenguni, akatezeka, akadhihakiwa, akapitia aibu na madharau, akasulubiwa msalabani kama mwizi, waka mchapa mijeledi, wakamdunga mkuki ubavuni, akasikia uchungu wa ajabu, Damu yake ikamwagika kama maji. kisa akawawa kinyama juu ya Msalaba? Alitenda kosa gani? Alifanya dhambi gani? La hasa, Yesu alikuwa mtakatifu. Haya yote aliyapitia kwa ajili yetu. Damu aliyo yamuaga ilikuwa kwa ajili ya ukombozi wetu.Tulipo ukumiwa kifo kwa sababu ya dhambi; "WARUMI 6:23; kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu bwana wetu" Sasa wewe utapona aje usipo itikia mwito huu wa wokofu ulio mgarimu Kristo Yesu mwana wa Mungu maisha yake? "Waibrania 2:3' Sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukadhitika kwetu na wale waliosikia
Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo ndiyo Fidia alio lipa kwa ajili ya ukombozi wetu, yaani kwa maneno mengine, tulinunuliwa kwa gara kuu sana ambayo hakuna mtu yeyote aliyekuwa na uwezo huo, duniani wala juu mbinguni.
DAMU YA YESU INANENA
Waibrania 12:24; Na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyiziwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.
DAMU YA YESU INANENA UPONYAJI
ISAYA 53:5; Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
DAMU YA YESU INANENA BARAKA
Wagalatia 3:13; Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; Maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti.
Mithali 10:22; Baraka ya Bwana hutajirisha, wala hachanganyi huzuni nayo
DAMU YA YESU UFUTA MAANDISHI YOTE YALIYOANDIKWA KINYUME CHETU
Wakolosai 2:14; Akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani.
DAMU YA YESU IMETUPATANISHA NA MUNGU
Dhambi ilitutenganiza na MUNGU muumba wetu, kifo kikaja duniani, mangonjwa ambayo hayana tiba ikaja duniani. Haya yote ni kwa sababu dhambi ili tutenganiza na Mungu, Mungu ni mtakatifu, kwahivyo hawezi kuchangamana na dhambi. Isaya 59:1-2; Tazama mkono wa Bwana haukupungukiwa, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia. Lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.
Kama ujampokea Kristo kuwa bwana na mwokozi wa maisha yako, ujuwe maisha yako ni matupu bila kinga nauko hatarini na kama mawindo kwa mkono wa mwindaji. Hii ndiyo maana Yesu alikuja ili atupatanishe na Mungu ili tuwe na kinga ya kutosha, maana mtu akiwa ndani ya kristo hakuna mipango ya adui iwezayo kufahulu maishani mwake. "Warumi 8:31; Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?"
Warumu 5:10; Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya mwana wake; Zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake.
Kama umesoma nakala hii naume okoka, tafadhali elendelea kutembea na Kristo kwa haki ukitakaswa kwa damu ya Yesu kila wakati mpaka Yesu atakapokuja kutunyakwa. Na kama hauja okoka, tafadhali chukua Bwana Yesu awe Bwana na Mwokozi wako kabla hauja chelewa Isaya 55:6; Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, mwiteni, maadamu yu karibu."