Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Yesu Kristo yu aja mara ya pili, na sis zote tutaondoka duniani. Kilicho cha maana kujiuliza ni kwamba; hatima yako itakuwa wapi baada ya kuondoka duniani?
Katika biblia kwa kitabu cha WAKOLOSAI 3:1-4; Hapo Mitume Paulo ana wandikia wakolosai baruwa akiwahimiza ya kwamba, wasiyafikirie mambo yaliyomo duniani, bali wayafikirie mambo yaliyo juu maana maisha yao umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.Paulo haneni tu na wakolosai, baali ananena na sisi zote kama kanisa la Yesu Kristo. Kwa maneno mengine, Paulo anasema ya kwamba mambo ya dunia hii yana mwisho wake, chochote ulicho nacho yanamwisho wake, na hata kama ni wewe utakapo funga macho na kuondoka duniani, yote uliyo navyo yote utayaacha hapa. Ndiyo maana Paulo anatuhimiza kwa hiyo barua yake kwa wakolosai akisema kwa haya ya pili; "yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi".
Katika kitabu cha MATHAYO 25:31-34, 41 Biblia inasema watu wote watakusanyika mbele ya kiti cha enzi ili wahukumiwe, na Kristo Yesu atawabagua, wengine mkono wake wa kulia, na wengine mkono wa kushoto. Kristo Yesu atawambia walio upande wa kushoto; ondokeni kwangu ninyi mlio waovu, kisa ata wakaribisha waliyo mkono wa kulia akiwaambia; karibuni mliyo tenda mema . Je wewe mpendwa utakuwa kwa mkono wa upande gani? je utakaribishwa na Yesu ama utafukushwa kwenda kwenye ziwa la moto?
Kitabu cha UFUNUO WA YOHANA 20:12, Biblia inasema; kutakuwa na vitabu viwili, kitabu kilichoandikwa majina ya waovu,watu wenye kutenda dhambi, hawa watahukumiwa kulingana na matendo yao na maneno ya vinywa vyao, wote watatupua katika ziwa la moto mahali pa kilio na kushaga meno. Kisa kitakuepo na kitabu kingine, walio andikwa ndani yake ni waliyo tenda mema, hao ndiyo watakaribishwa mbinguni katika uzima wa milele. Je, wewe utakuwa wapi? Jina lako litapatikana kwa kitabu gani? Tafadhali mpendwa wangu, tayarisha hatima yako ungalipo hai, hamua wakati huu ungalipo hai kama utakuwa pamoja na Kristo Yesu mbinguni, ama kwenye ziwa iwakao moto.
MHUBIRI 12:13-14, Hii ndiyo jumla ya maneno; Yote yamekwisha sikiwa; mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.
Mpendwa wangu, acha dhambi, tubu na umgeukie Mungu, Yesu yuaja hivi karibuni, usije ukajipata pabaya.