Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
ZABURI 121:1-4
Daudi alikuwa mwimbaji hodari, alitunga nyimbo nyingi sana ya kumsifu Mwenyezi Mungu.
Kwenye kitabu hiki cha cha Zaburi 121 Daudi anatuhubiria ujumbe wa hakikisho la ulinzi wa Mungu kupitia wimbo huu wa Zaburi. Msitari wa 1 anajiulisa maswali akisema; Nitayainua macho yangu nitazame milima, msaada wangu utatoka wapi?
Msitari wa 2 anajibu akisema; Msaada wangu u katika BWANA aliyezifanya mbingu na nchi.
Daudi aligundua siri kumtafuta Mungu wakati wa mateso, ndiyo maana akaangalia duniani kote, hakupata msaada popote. Mpendwa wangu nataka nikuambie, suluhizo ya shida yako haliko duniani wala kwa mwanadamu, mleete Yesu shida yako, maana yeye ndiye msaada wa kweli. Mwanadamu atakusaidia atimaye atachoka alafu msaada wake itakoma, wengine watakusaidia nawakuweke vikwazo. Lakini YESU hanavikwazo, anacho taka tu ni wewe umpoke kuwa bwana na Mwokozi wa maisha yako.
Katika kitabu cha Mathayo 11:28, Kristo Yesu anasema; Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na misigo, nami nitawapumzisha .kwake YESU, ndiko tuna tua msigo zetu zote. Misigo ya magonjwa, misigo ya majaribio mbalimbali, misigo ya taabu zetu. Kila aina ya misigo maishani mwako, mletee Kristo Yesu, Maana yeye ndiye msaada wa kweli. Hakuna ajaye kwake amemtupa, yeye atakupokea na akuondole misigo uliyomsito maishani mwako.
Kwahivyo mpendwa, ukitaka Yesu awe msaada wako, lazima umpoke awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Leo hii ukisikia sauti yake usifanye moyo wako kuwa mgumu. Mkubali Yesu, upate msaada na pumziko maishani mwako.