Ijapo Mungu anatupenda na upendo wanamna hii, tusisahau ya kwamba anachukia dhambi wala hauziki na dhambi. kwahivyo ukiruhusu dhambi ikutawale, dhambi itaweka mpaka kati yako na Mungu. Kwahivyo acha dhambi ili uishi maisha matakatifu.
Kuishi chini ya mamlaka ya ulimwengu inamanisha mambo unayo yafanya ni ya kiulimwengu yasiyo mpendeza Mungu. Kwa njia nyingine inamanisha, maisha yako yana fanana na ya wale ambayo hawaja mtambua Kristo.
Neno la Mungu lina nguvu, uwezo na mamlaka. kuanzia kitabu cha mwanzo hadi ufunuo limejaa neno. Kuna tofauti kati ya maneno na Neno; maneno ni ya mwanadamu, ila Neno ni la Mungu.
Mahali pa muhimu kuka ni katika uwepo wa Mwenyezi Mungu, Hilo ndilo siri ambayo Daudi aligundua, Daudi alidumu uweponi pa Mwenyezi Mungu. Kwahivyo tukidumu katika uwepo wa Mungu, tutakuwa salama.
Silaha ni chombo kilichoundwa kwa ajili ya vita, na inatumika kwa ajili ya ulinzi na kukabiliana na maadui. Kwenye fasiri la kingeresa ukisoma hilo kitabu cha YEREMIA 51:20 katika toleo la mfalme Yakobo, inasungumza kuhusu SHOKA.